Moto wazidi kuchoma msitu Ufaransa
Hali isiyotarajiwa ya upepo, joto na kiangazi kikali Kusini Mashariki mwa Ufaransa, imechangia kuenea kwa kasi kwa moto wa msituni, kote katika eneo hilo.
Wazima moto 600 wanakabiliana na moto huo ambao ulianza Jumatatu asubuhi, katika mbuga moja ya kitaifa ya wanyama pori, iliyoko katika jimbo la Luberon, na kufikia sasa moto huo unateketeza eneo la ukubwa wa kilomita 8 mraba.
- Idadi ya waliouawa na moto wa nyika yafika 62 Ureno
- Jeshi kusaidia kuzima moto Canada
- Moto waangamiza mji Chile
Mamia ya watu wamehamishwa kama njia ya kuchukua tahadhari




No comments