Tetesi za usajil majuu mchana uhu

Bayern Munich itakuwa inamuangalia kwa makini kipa wa Everton na England Jordan Pickford, mwenye umri wa miaka 24, katika kombe la dunia mwezi huu. (Sun)
Liverpool inaendelea kumwinda mchezaji wa kiungo cha kati wa Lyon mwenye thamani ya £ milioni 60 Nabil Fekir, licha ya kwamba ripoti kuhusu mazungumzo na ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Jumapili ni ya mapema. (Liverpool Echo)
Kipa wa Roma na Brazil Alisson, mwenye umri wa miaka 25, atakataa kujiunga na Liverpool ili kusubiri uhamishoni kwa Real Madrid. (Marca - via Mail)
Arsenal inamlenga Stephan Lichtsteiner beki wa kulia mwenye umri wa miaka 34 raia wa Uswisi ambaye kandarasi yake Juventus inamalizika msimu huu wa joto, amesisitiza kwamba mkataba wa kujiunga na Emirate haujakamilika. (London Evening Standard)
Meneja mpya wa Everton Marco Silva anatayarisha ombi la £ milioni 30 kumsajili kapteni wa Newcastle Jamaal Lascelles, mwenye umri wa miaka 24. (Sun)
Silva hajakaa kwa zaidi ya mziu mmoja katika klabu tatu alizozisimamia tangu aondoke EstorilHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Image captionSilva hajakaa kwa zaidi ya mziu mmoja katika klabu tatu alizozisimamia tangu aondoke Estoril
Huddersfield wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa AC Milan raia wa Ureno Andre Silva, mwenye umri wa miaka 22. (Sky Sports)
Santi Cazorla, mwenye umri wa miaka 33, anajifunza na timu ya vijana katika ligi ya Uhispania Alaves baada ya kuondoka Arsenal. Mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Uhispania huenda pia akaanza kufanya mazoezi na Villarreal. (London Evening Standard)
Winga wa Uswisi Xherdan Shaqiri, 26, amethibitisha ataondoka katika timu ya Stoke iliyoshuka daraja msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wamiaka 26 anataka kujisajili katika klabu iliopo katika ligi ya England (Aargauer Zeitung - via Stoke Sentinel)
Fulham itafanya mazungumzo na kocha mkuu Slavisa Jokanovic kuhusu mktaba mpya atakaporudi kutoka mapumzikoni. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 49 amesalia na mwaka mmoja katika mktaba wake. (Times )
Besiktas wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Everton Davy Klaassen, 25. Klabu hiyo ya Uturuki inataka kumchukua Klaassen kwa mkataba wa awali wa mkopo. (Sky Sports)
Leicester na Southampton wanamwinda winga wa Lazio Felipe Anderson, anaye nong'onezewa kulengwa kwa thamani ya £ milioni 35 na West Ham. (Tuttosport, via Leicester Mercury)
Watford inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kwa thamani ya Euro milioni 10 beki wa kushoto wa Bologna Adam Masina, mwenye umri wa miaka 24. (Watford Observer)
Mlinzi wa Sunderland Paddy McNairHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMlinzi wa Sunderland Paddy McNair
Brighton itaongeza thamani ya ombi lao kwa mlinzi wa Sunderland Paddy McNair. Mpaka sasa wamewasilisha maombi mawili yaliokataliwa kumsajili mchezaji huyo mweny umri wa miaka 23. (Sunderland Echo)
Brighton itapambana na Everton kumsajili kwa thamani ya £ milioni 5 ya mlinzi chipukizi wa Charlton Ezri Konsa, mwenye umri wa miaka 20. (Mirror)
Real Madrid inataka kufanya usajili wa haraka kuziba pengo analoacha Zinedine Zidane baada ya kukubali kushindwa katika kumsajili meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino. (Daily Mail)
Arsene Wenger anasema hana hakika iwapo anataka changamoto nyingine nzito wakati kocha huyo mwnye umri wa miaka 68 akitafakari hatua atakayopiga baada ya kuondoka Arsenal. (London Evening Standard)
Wenger alionekana na familia yake na marafiki Jumamosi akibariziHaki miliki ya pichaZSOFI ZSARNAI
Image captionWenger alionekana na familia yake na marafiki Jumamosi akibarizi
Wenger anaamini aliyekuwa mchezajiw a Arsenal Patrick Vieira atakuwa kiongozi mkuu - iwapo atajitolea 'maisha yake'. (Mirror)
Meneja wa Rangers Steven Gerrard ana hamu kumsajili mchezaji chipukizi wa kiungo cha kati wa Liverpool Ovie Ejaria. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alichukuliwa kwa mkopo Sunderland mwaka jana. (Sun)
Beki wa Fulham Ryan Fredericks amekataa ombi la mkataba mpya na Craven Cottage kwasababu anataka kuwa mchezaji anayelipwa kiwango kikubwa cha pesa katika klabu hiyo. Aanatarajiwa sasa kujiunga na West Ham. (Football.London)

No comments

Powered by Blogger.