Msichana wa kipalestina aliyempiga mwanajeshi wa Israel akamatwa
Mamlaka za Israel zimemfungulia mashtaka msichana mpalestina ambaye alirekodiwa kwenye video akimshambulia mwanajeshi wa Israel.
Ahed Tamimi, 17, na binamu yake walirekodiwa kwenye video wakiwakabili wanajeshi wa Israel katika kanda iliyosambaa pakubwa katika mitandao ya kijamii.
Anakabiliwa na kesi 12 ikiwemo dhuluma na kurusha mawe.
Lakini familia yake inasema kuwa walihusika kwenye maandamano katika eneo linalokaliwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.
- Wapalestina wamuita balozi wao kutoka Marekani
- Mwanajeshi wa Israel miezi 18 jela kwa kumuua Mpalestina
- Jerusalem: Mataifa ya kiarabu yalaani hatua ya Marekani
Jeshi la Israel linasema kuwa wanajeshi hao walikuwa wakiwazuia wapalestina kutokana na kurusha mawe kwa waendesha magari.
Video hiyo iyorekodiwa tarehe 15 Disemba ilionyesha kikundi cha wanawake akiwemo Tamini, wakiwapiga wanajeshi wawili wa Israel waliokuwa wamejihami vikali.
Ilisambaa sana katika mitandao na wapalestina wengi wamemsifu Tamini kuwa shujaa kwa kuipinga Israel.
No comments