Croatia imeanza kwa kutoa kichapo kizito kuelekea kombe la dunia

Timu ya taifa ya Croatia imepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ugiriki katika mchezo wa mtoano wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.
Magoli ya Croatia yalifungwa na Luka Modric aliyefunga kwa mkwaju wa penati, Nikola Kalinic akaongeza goli la pili, mshambuliaji Ivan Perisic akaongeza goli la tatu.
Mshambuliaji Andrej Kramaric akahitimisha kazi kwa goli na nne goli pekee la Urigiki katika mchezo huo lilifungwa na Sokratis Papastathopoulos
Switzerland wakicheza ugenini wamewafunga Ireland Kaskazini kwa bao 1-0 bao lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Ricardo Rodriguez.
Michezo ya Marudiano kwa timu hizi itachezwa Novemba 12 na washindi wa jumla watafuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia.

No comments

Powered by Blogger.