Matokeo Kenya yasubiliwa kwa hamu
Muhtasari
- Tume ya Uchaguzi inaendelea kupokea Fomu 34A za matokeo ya urais kutoka vituoni
- Matokeo ya awali yanaonesha Rais Kenyatta anaongoza akiwa na kura 8 milioni. naye Bw Odinga ana kura 6.6 milioni.
- IEBC imesema mitambo yake haidukuliwa, kinyume na madai ya muungano wa upinzani Nasa
- Jumanne kulitokea vurugu katika baadhi ya maeneo mtaa wa Mathare, Nairobi na baadhi ya maeneo Kisumu. Lakini kwa sasa hali ni tulivu
- Waziri wa usalama Fred Matiang'i amewaomba wananchi kuendelea na shughuli za kawaida bila wasiwasi
- Katika barabara za Nairobi magari yameanza kuonekana lakini bado hali ya kawaida haijarejea
Habari za moja kwa moja
Ulikuwa ni usiku wa shughuli nyingi katika kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo Bomas.
Maajenti wa vyama vya siasa walikuwa wakikagua Fomu 34A za matokeo kutoka vituo vya kupigia kura katika sehemu maalum.
Mgombea wa upinzani Raila Odinga alikuwa amelalamika awali kwamba IEBC ilikuwa ikitangaza matokeo bila kutoa fomu hizo.
Tume hiyo baadaye ilitoa fomu hizo. Kufikia sasa ni vituo 1,200 pekee kati ya 40,883 ambavyo havikuwa vimewasilisha fomu hizo.
Tume ya uchaguzi imeahidi kutoa maelezo kuhusu matokeo yaliyo kwenye fomu zilizopokelewa Bomas baadaye leo.
Soma zaidi:
BBC
BBC
BBC
Mwandishi wa BBC Abdinoor Aden alikuwa ukumbi wa Bomas usiku ambapo maafisa wakuu wa tume ya uchaguzi wanajumlishia matokeo na kutoa taarifa kuhusiana na uchaguzi.
Mtazame hapa kuhusu yaliyojiri:
No comments