Watu wawili wauwa Jordan na muisraeli moja kujeruhiwa
Watu wawili raia wa Jordan wameuawa na muisrael mmoja kujeruhiwa wakati wa kisa cha ufyatuaji risasi kwenye ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Jordan Amman.
Watu hao walikuwa wakifanya kazi na kampuni moja ya zamani na waliingia ndani ya ubalozi kabla ya ufyatuaji risasi kuanza kwa mujibu wa polisi.
Ripoti chache zimetolewa kuhusu kile kilisababisha kutokea kwa ufyatuaji huo wa risasi.
Vikosi vya usalama vimezingira ubalozi huo na utawala wa Israel umewahamisha wafanyakazi.
Ufyatuaji huo ulitokea katika jengo moja linalotumiwa na ubalozi wa Israel.
- Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem
- Polisi wawili wa Israel wauawa Jerusalem
- Israel kujenga nyumba 560 mashariki mwa Jerusalem
Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho.
Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman.
Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.

No comments