Marekani yaionya Syria kuhusu shambulio la kemikali
Marekani inasema kuwa imetambua maandalizi muhimu ya shambulio jingine la kemikali nchini Syria na kutoa onyo kali kwa serikali ya Syria.
Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa vitendo hivyo ni sawa na vile vilivyokuwa vikifanywa kabla ya shambulio la kemikali mnamo mwezi Aprili.
Makumi waliuawa katika shambulio hilo na kumlazimu rais Barrack Obama kutekeleza shambulio dhidi ya kambi moja ya majeshi ya Syria.
Taarifa hiyo ya Syria ilimuonya rais Bashar al Assad kwamba atakiona cha mtema kuni iwapo shambulio jingine litafanyika.
Imesema kuwa shambulio jingine la kemikali litakalotekelezwa na utawala wa Assad litasababisha mauaji ya raia wengi.
Taarifa hiyo iliongeza: Kama tulivyosema hapo awali ,Marekani iko nchini Syria kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State kutoka Iraq na Syria.
Hatahivyo iwapo Assad atatekeleza shambulio jingine la kemikali yeye na jeshi lake watakiona cha mtema kuni.
No comments