Magufuri kawalaza chini wapinzani
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba amefunguka na kusema kuwa Rais Magufuli ameshawalaza chini wapinzani wote na kutegua mitego yao kwani kila kichaka wanachokwenda kujificha anawaona na kukisambalatisha.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Mwigulu Nchemba amesema kuwa viongozi wa taifa hili hawajawahi kuwa Ma- Agent wa watu au mataifa yanayoliibia taifa bali watu ambao wanawatetea wezi ndiyo maanjeti wa wezi hao wanaliibia taifa madini na maliasili zake.
"Wale wenye nia mbaya wametafuta vichaka vingi sana lakini kila kichaka wakijaribu na chenyewe kinayeyuka, walisema tutashtakiwa hivi siku hizi mwizi naye anashtaki aliyemwibia? Kichaka hicho kikayeyuka Mwanzoni walikuwa wanasema mchanga tu hauna kitu lakini hili wala halihitaji shule kujua kama ni mchanga tu hauna kitu hawa watu wangekuwa wanakuja kuchukua mchanga tu kila siku. Kwa hiyo hawa watu walikuwa wanatuona kama mazuzu tu lakini Rais wetu amechukua hatua tena si kwa maneno kwa vitendo tumuunge mkono" alisema Mwigulu Nchemba
Waziri Mwigulu aliendelea kusisitiza
"Walipoona kichaka hicho kimekwama wakaanza kutaja viongozi kuwa wanahusika wakidhania hiyo itakuwa kitu cha kuzuia ili jitihada hizo zisiendelee wakaanza kutaja na viongozi wastaafu hiyo yote si kama walikuwa wanataja kuwa viongozi hao wanahusika bali walikuwa wanataka itumike kama kichaka kwamba tukitaja viongozi hao wataacha , mimi niwaambie viongozi wetu hawa hawajawahi kuwa Ma- Agent wa wale wanaotuibia bali wale wanaotetea wezi ambao tumewaona ndiyo Ma- Agent wa wezi hao, na Rais akauona huo mtego akautegua sasa hivi kama ni gari lao lile basi matairi yote Rais Magufuli ameshatoa upepo, yameshalala chini" alisisitiza Mwigulu Nchemba
Mbali na hilo Mwigulu Nchemba alizidi kuwaomba watanzania waendelee kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kutumbua na kutegua mitego hiyo ya wapinzani na watetezi wa wezi wa maliasili za nchi.
No comments