Waziri George simbachawene amewaonya wasimamizi Wa mitiani ya taifa kitado cha sita

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. George Simbachawene amewaonya wasimamizi wa mitihani ya taifa ya kidato cha sita pamoja na wahitimu walioanza kutahiniwa leo nchini kote, amewataka kutofanya udanganyifu kwa lengo la kurahisisha ufaulu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. George Simbachawene
Simbachawene amesema kuwa tabia ya wasimamizi kuwafanyia mtihani baadhi ya watahiniwa, inatakiwa isiwepo kabisa katika mitihani hiyo, bali wanapaswa kuhakikisha wanazingatia kanuni na taratibu kwa kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote.
Mbali na hilo Simbachawene amesema wasimamizi wa mitihani wa ngazi za mikoa, wilaya, halmashauri na shule, wanatakiwa kusimamia na kuendesha mitihani kwa weledi, uadilifu na uaminifu kwa muda wote kuanzia Mei 2 hadi Mei 19, mwaka huu.
Hata hivyo, Simbachawene amesema hakuna taarifa zozote za kuwapo na udanganyifu toka kwa wasimamizi na watahiniwa hao.
Jumla ya wanafunzi 75,155 wakiwamo wavulana 46,406 na wasichana 28,749, wameanza mitihani yao katika vituo 577 vilivyopo nchi nzima.

No comments

Powered by Blogger.