Ozil kasain mkataba mpya Giroud Chelsea Aubamiyang arsenal Batshuayi Dortmund
Borussia Dortmund imekubali mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi kwa mkopo kwa kipindi cha msimu uliosalia, akisubiri kufanyiwa matibabu.
Arsenal ilimsajili mshambuliaji Pierre Emeric Aubameyang ambaye Dortmund wanasema watamuuza tu iwapo watapa mchezaji mwengine kuchukua mahala pake.
Chelsea huenda ikamsajili Olivier Giroud kutoka Arsenal ili kuchukua mahala pake Batshuayi ili kukamilisha mkataba wa miaka mitatu.
- Mesut Ozil donge nono-Arsenal
- Mesut Ozil kuuzwa asiposaini mkataba
- Arsenal yasitisha mazungumzo na Sanchez na Ozil
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil ametia saini kandarasi ya miaka mitatu na nusu ili kusalia katika klabu hiyo hadi 2021.
![Mitchy Batshuayi](https://ichef-1.bbci.co.uk/news/375/cpsprodpb/14639/production/_99831538_96f37210-7ef0-45d8-9fc9-41a828c2ec1a.jpg)
Ozil mwenye umri wa miaka 29 sasa ndio mchezaji anayepokea mshahara mkubwa katika klabu hiyo akijapatia kitita cha £350,000 kwa wiki kabla ya kulipa kodi.
Mkataba huo uliotiwa saini siku ya Jumatano, unajiri baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuhusu hatma ya raia huyo wa Ujerumani ambaye kandarasi yake ya awali ilikuwa inakaribia kuisha mwishoni mwa msimu huu.
- Wachezaji wawili wanaomzuia Aubameyang kutua Arsenal kwa sasa
- Chelsea yailaza Atletico Madrid ugenini
Alijiunga na Gunners kutoka Real Madrid 2013 kwa rekodi ya uhamisho wa dau la £42.4m.
No comments