Caribbean ya jiandaa kwa kimbunga kingine kikubwa
Kimbunga Maria kinatarajiwa kuwa kibunga hatari wakati kinakaribia visiwa vya Leeward eneo la Caribbean.
Kimbunga hicho cha kiwango cha kwanza kitapata nguvu kwa haraka ndani ya saa 48 zinazokuja na kugonga visiwa hivyo baadaye leo Jumatatu.
Kimbunga hicho kinapitia eneo ambalo kimbunga Irma kilipitia.

Onyo la kimbunga limetolewa maeneo ya Guadeloupe, Dominica, St Kitts na Nevis, Montserrat na Martinique.
Tahadhari ya kimbunga kwa sasa inachukuliwa nchini Marekani na visiwa vya Uingereza vya Virgin, St Martin, St Barts, Saba, St Eustatius na Anguilla.

Baadhi ya visiwa hivyo bado vinajaribu kurejea hali ya kawadia baada ya kupigwa na kimbunga cha kiwango cha tano, kilichosababisha vifo vya takriban watu 37 na hasara ya mabilioni ya dola.

Kwa mujibu wa utabiri wa kwanza kimbunga Maria kitapitia visiwa vya Leeward baadaye Jumatatu na Jumatatu usiku kisha kielekee maeneo ya kusini mashariki mwa bahari ya Caribbean siku ya Jumanne na Jumanne usiku.

No comments