Barcelona yaandika historia ligi ya mabigwa ulaya

Barcelona wamebirua matokeo ya kutinga nusu fainali kwa kuizaba Paris Saint Germain kwa mabao 6-1 katika mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa Ulaya.
BarcaHaki miliki ya pichaLAURENCE GRIFFITHS
Image captionNeymar alin'gara katika mchezo huu
Sergi Roberto alifunga bao la 6 kwa mkwaju wa mwisho wa mchezo, na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 6-5 kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp.
Barcelona walifunga magoli matatu katika dakika saba za mwisho. Walikuwa wakiongoza kwa 3-1. Wiki tatu zilizopita PSG iliifunga Barcelona magoli 4-0 mjini Paris.
Hatua ya kurejesha magoli yote hayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya soka, na sasa Barcelona wana kila nafasi ya kunyanyua kombe la Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
Katika mchezo mwingine, Pierre Emerick Aubameyang alipachika 'hat trick' na kuipeleka Borussia Dortmund katika robo fainali dhidi ya Benfica.
DortmundHaki miliki ya pichaFRIEDEMANN VOGEL
Image captionAubameyang alifunga magoli matatu
Borussia Dortmund wameshinda kwa jumla ya magoli 4-1 katika mechi mbili walizocheza.

No comments

Powered by Blogger.