Vituo 40 vya matibabu vya sitishwa Tanzania
Serikali ya Tanzania imesitisha huduma za msaada kwa vituo 40 vya matibabu vinavyodaiwa kuwasaidia wapenzi wa jinsia moja kulingana na chombo cha habari cha AP.
Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini humo na wanaopatikana na hatia hupigwa faini ya miaka 30 jela.
Serikali inaamini kwamba mashirika yasiokuwa ya kiserikali NGOs hutumia vituo hivyo vya afya kukuza mapenzi ya jinsia moja, Kulingana na chombo cha habari cha AP kilichomnukuu waziri wa afya Ummi Mwalimu.
- Watoto wa Tanzania wana afya nzuri ya maungo duniani
- Ndege zisizo na rubani kutoa huduma za tiba Tanzania
Waziri wa afya pia alitangaza kwamba serikali inaongeza takriban vituo 3000 vya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya ukimwi nchini humo, imeongezea AP.
AP imeongezea mwezi Septemba kwamba serikali itasimamisha kwa muda huduma ya mipango ya kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya ukimwi inayolenga wapenzi wa jinsia moja.
No comments