Shirika la Amnesty International limemshutumu Trump
Shirika la Amnesty International limemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump na viongozi wengine nchini Uturuki, Hungary na Ufilipino.
Shirika hilo limesema viongozi hao wanaendeleza kile inachokitaja kuwa kuwatumia vibaya wakimbizi, kwa manufaa yao ya kisiasa, badala ya kutanzua kiini hasa kilichowafanya wakimbizi hao kuyakimbia mataifa yao.
Katika ripoti yake ya kila mwaka, Amnesty inaelezea mwaka 2016, kama mwaka wa matamshi yaliyojaa chuki huku hofu ikapanda zaidi na kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikia tangu miaka ya 1930, wakati Adolf Hitler, alipoingia uongozini nchini Ujerumani.

Ripoti hiyo inapinga sera ambazo zinakubalia ubaguzi wa rangi na chuki.
Inasema mataifa mbalimbali duniani yanaendesha ajenda potovu ambayo inawahujumu wakimbizi ambao wanashutumiwa kwa makosa ambayo hawakutenda huku pia wakidhulumiwa kijumla.
No comments