Leicester city waitimbua mipango ya Liverpool jana
Leicester City wamejikokota na kupanda hadi nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuizaba Liverpool kwa mabao 3-1.
Leicester walionesha kiwango cha juu, na magoli mawili kutoka kwa Jamie Vardy na moja kutoka kwa Danny Drinkwater yaliididimiza Liverpool.
Wakicheza chini ya kaimu kocha Craig Shakespeare, aliyechukua mikoba ya Ranieri, mabingwa hao wa England walicheza kama mabingwa watetezi.
- Ranieri aongeza mkataba Leicester City
- Ranieri atumai Leicester watafana UEFA
- Mourinho: Wachezaji wenye ubinafsi walimsaliti Ranieri
Goli la kwanza la Jamie Vadry limekumbusha mtindo waliokuwa wakicheza msimu uliopita, baada ya pasi murua kutoka kwa Marc Albrighton iliyomfikia Vardy.
Magoli haya ya Leicester ndio magoli ya kwanza kwa klabu hiyo kufunga mwaka huu wa 2017.
Liverpool ambao wangeweza kupanda hadi nafasi ya tatu iwapo wangepata ushindi, sasa wamepoteza mechi tano kati ya saba walizocheza katika michuano yote.
No comments